Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan Kusini Taban Deng ambaye yuko ziarani nchini Afrika Kusini amesema, Sudan Kusini inatekeleza amani kwa sababu nchi hiyo haina uamuzi mbadala.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Cape Town baada ya mazungumzo kati yake na makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, Deng amesema ni lazima kuwe na utulivu ili wananchi waweze kuendelea, kupata huduma za afya, kuwa na uhakika wa chakula na miundombinu bora ya barabara. Amesema serikali yake iko makini sana katika utekelezaji wa amani, na kwamba nchi hiyo haitarudi tena kwenye mgogoro au vita.
Kwa upande wake, makamu wa rais wa Afrika Kusini Ramaphosa amesema, kwa sasa serikali ya Sudan Kusini imekuwa imara, bunge limeanza kufanya vikao vyake, na hayo ni maendeleo yanayotakiwa kupongezwa. Amesema kuwa nchi yake na Sudan Kusini zimekubaliana kuunda kikosi kazi kitakachoshughulika na masuala yanayogusa maslahi ya pande hizo mbili.

Post a Comment

 
Top