BILIONEA Mohammed Dewji ‘Mo’, amelitazama soka la Simba iliyoibamiza AFC Leopards ya Kenya kwa mabao 4-0 na kuelezwa kwamba zimebaki siku 11 tu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Unajua amewauliza nini mabosi wa klabu hiyo? Tayari mmekwishapata mdhamini?Mabosi hao waliposhindwa kumjibu akawapa muda wa siku tatu wawe wamempa mchanganuo ili kampuni yake iweze kuingia mkataba wa udhamini na klabu hiyo.Na habari za uhakika ni kwamba, Kamati ya Utendaji ya Simba imeondoa mzizi wa fitinaambapo jana ilitarajia kukutana kwa ajili ya maamuzi ya kutafuta mdhamini kufuatia kujiondoa kwa Kampuni ya TBL ambapo katika maamuzi hayo wameamua kumkabidhi timu hiyo Mo.Taarifa za ndani kutoka Simba zinadai kuwaKamati ya utendaji kwa kauli moja inataka kumpa Mo majukumu mazito ya kuiongoza timu hiyo wakati huu ambao wanaendelea na mchakato wao wa kumpa hisa.TBL iliamua kusitisha mkataba wake na Simba baada ya watani zao wa jadi Yanga kukataa udhamini huo ambao ulikuwa unazihusu timu hizo mbili peke yao.Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Simba umeona ni bora kumkabidhi mwanachama wao huyo kuendelea kutoa mchango wake wa hali na mali wakati huu wakiendelea kukamilisha suala lililopo mbele yao la kumpa hisa asilimia 51.Mo ameshatangaza kutaka kuweka hisa ya asilimia 51 yenye thamani ya Sh bilioni 20 ambapo wanachama wameshalipitisha katika mkutano wao mkuu na sasa kinachosubiriwa ni uongozi kuweka mambosawa.Kigogo mmoja aliliambia DIMBA Jumatano kuwa ndani ya wiki hii, Mo atakabidhiwa majukumu hayo ya kuwa mdhamini kwa muda, lengo kubwa likiwa kuhakikisha mambo yao yanakwenda kama walivyoyapanga.“Ni kweli suala hilo lipo na Kamati ya Utendaji itakutana kuliangalia hilo na kuna kila dalili akakabidhiwa kuwa mdhamini katika kipindi hiki baada ya mkataba wetu na TBL kufikia kikomo.“Nadhani siku mbili hizi kila kitu kinaweza kuwa hadharani, tunachowaomba mashabiki wetu wote duniani ni kuiunga mkono timu yao kwani dhamira yetu ni kutwaa ubingwa msimu ujao,” alisema kigogo huyo.Mtoa habari huyo alisema kwa mantiki hiyo huenda Mo akaingia kupitia kampuni yake ya Mohammed Enterprises Limited (MeTL).Hakuna kiongozi wa Simba aliyekuwa tayarikulizungumzia suala hilo na hata gazeti hili lilipojaribu kuwatafuta kwa simu, ziliita bila majibu.
Home
»
»Unlabelled
» MO HATIMAYE APEWA TIMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment