Kocha wa Yanga George Lwandamina,  na viongozi wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo wako katika mtihani mzito kuliko wakati wowote wakitaka saini za nyota wawili Papy Kabamba Tshishimbi, wa Mbabane Swallows na Cletus Chama wa Zesco ya Zambia.

Lwandamina amesema katika machaguo hayo mawili anamuhitaji mchezaji mmoja ambaye ataziba vyema nafasi ya kiungo Haruna Niyonzima, aliyeondoka kwenye klabu hiyo na kujinga na mabingwa wa Kombe la FA, Simba.

“Wote ni wachezaji wazuri nawajua vizuri lakini kuna tofauti  moja ya uumri hapo ndipo nitakapopaangalia vizuri maana kuwa na mchezaji mwenye umri mdogo inakupa anakupa uhakika wa kuweza kupambana kwa asilimia 95 tofauti na mchezaji mwenye umri mdogo,”amesema Lwandamina.

Kocha huyo amesema kutokana na hilo atamuhitaji zaidi Chama, kwasababu ni mchezaji mzuri anauwezo wa kukaba lakini pia kuichezesha timu na kufanya mashambulizi  hivyo ni mtu ambaye anampa kipaumbele.

 Kwaupande wake Hussein Nyika, amesema wanalifanyia kazi swala la kocha wao Lwandamina na kupambana kadri ya uwezo wao  ili waweze kumnasa mchezaji huyo kwa ajili ya maslahi ya timu yao.

“Ngoja tupambane kuona kama tutalifanikisha hilo, na baada ya dirisha kufungwa tutajua kama tumefanikiwa au vinginevyo lakini Kamati yangu imekusudia kumchukua mchezaji huyo ili kutimiza agizo la kocha Lwandamina.

Yanga tayari imemsajili mchezaji mmoja wa kigeni ambe ni kipa wa African Lyon Rostand hali inayoacha nafasi mbili tu za wachezaji kutoka nje ya nchi ambayo kwa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinapaswa kujazwa na kiungo mmoja na beki wa kati mmoja.

Post a Comment

 
Top