Meneja wa klabu ya Celtic ya Scotland Brendan Rogers amesema mchezaji wa klabu ya Barcelona ya Uhispania Luis Suarez ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani.
Rogers, akizungumza kabla ya mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kati ya klabu hizo mbili baadaye Jumanne amemtaja Suarez kama mchezaji mtanashati mnyenyekevu mwenye bidii sana na mtu wa familia, ambaye hujitolea kwa hali na mali kwa soka na familia.
Suarez alichezea Liverpool Rogers alipokuwa meneja na kuihama klabu hiyo mwaka 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment