Uongozi wa klabu ya Azam FC umekubali kucheza mchezo wake wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, dhidi ya Simba, kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Jumamosi hii.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Karume, jijini Dar es Salaam, Afisa Habari wa shirikisho hilo, Alfred Lucas, amesema TFF ilikaa na Azam, na timu hiyo, kuomba kuhamishia mchezo huo, kutoka uwanja wa Chamazi kuja uwanja wa Uhuru.

Post a Comment

 
Top