Mgombea urais nchini Marekani kwa chama cha Democrat Hilary Clinton amefutilia mbali mikutano yake ya kampeni iliyokuwa imeratibiwa kuanza Jumatatu katika jimbo la Carlifornia baada ya kuugua maradhi ya nimonia.
Clinton alilazimika kuenda kwa nyumba ya binti wake mjini New York baada ya kulemewa na makali ya nimonia na kuondoka mapema kwenye hafla ya ukumbusho wa shambulizi la kigaidi la Septemba 11 iliyokuwa ikiendela mjini humo, Jumapili.
Mojawapo ya mikutano iliyofutwa ni ya kuchangisha pesa za kampeni ambapo mwanamuziki mashuhuri Lionel Richie angetumbuiza watu kwa nyimbo zake siku ya Jumanne. Wanaohudhuria hafla hiyo wangetakikana kulipa kuanzia dola $ 5,000 kwa njia ya tiketi huku wanaotaka kukaa karibu na Clinton na hata kupiga picha na yeye wakileta mchango wa hadi dola $ 50,000.
Post a Comment