TAHADHARI kutoka TFF. Kwa Majimaji ya Songea, Mwadui ya Shinyanga, Mbeya City ya Mbeya, African Lyon ya Dar na Mbao FC ya Mwanza.
1. Mchezaji anayefahamika kwa majina ya George Mpole ambaye ndiye Gerard Mpole wa Majimaji ya Songea, amefungiwa kucheza soka kwa mwaka mmoja kwa kosa la kubadili jina akiwa na lengo kufanya udanganyifu kwenye usajili. Mchezaji huyo kutoka Kimondo FC. Majimaji isimtumie.
2. Mchezaji William Lucian aliyesajiliwa Mwadui ya Shinyanga kutoka Ndanda ya Mtwara, naye amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kusajili timu nyingine ilihali akiwa na mkataba na timu ya zamani. Mwadui isimtumie mchezaji huyu.
3.Mchezaji Said Mkopi pia amefungiwa mwaka mmoja kwa kosa la kusajili timu mbili. Imebainika ana mkataba na Tanzania Prisons ya Mbeya na hapohapo amesajiliwa na Mbeya City. Mbeya City isimtumie mchezaji huyo.
4. Mchezaji Rehani Kibingu aliyesajiliwa African Lyon ya Dar, amesimamishwa mpaka uongozi wa timu African Lyon utakapomalizana na Ashanti United ya Dar kabla ya Agosti 27, 2016. African Lyon, isimtumie mchezaji huyu.
5. Emmanuel Kichiba aliyesajiliwa Mbao FC naye amesimamishwa mpaka Mbao watakapomalizana na Ashanti Utd kabla ya Agosti 27, 2016. Taarifa hii kutoka Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ni rasmi ikitolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF,  Alfred Lucas. Baadaye unaweza kutembelea website ya TFF.

Post a Comment

 
Top