Katibu mkuu wa klabu ya Yanga, Boniface Mkwasa amesema viongozi wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) wamekuwa wakiipendelea Simba katika upangaji wa ratiba za mechi.

Mkwasa amesema ilipaswa wao wacheze kesho na Mwadui katika uwanja wa taifa lakini wamepangiwa Uhuru wakati Simba keshokutwa itacheza na Singida United kwenye dimba hilo.

"Kama mnakumbuka hata kwenye mchezo wetu dhidi ya Tanzania Prisons tulipelekwa Azam Complex wakati Simba ilicheza na Lipuli siku ya pili uwanja wa Uhuru sidhani kama jambo hilo ni sawa.

"Kesho sisi tutacheza na Mwadui uwanja wa Uhuru, keshokutwa wenzetu Simba wanacheza uwanja wa Taifa hapo hakuna usawa kabisa," alimaza Mkwasa.

Katibu huyo alisema pia mchezo wao wa klabu bingwa Afrika dhidi ya St Louis ya Shelisheli utafanyika Jumamosi ya Februari 10 katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top