Manchester City wameamua kuacha kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez. City wameona gharama ya kumsajili mchezaji huyo ni kubwa sana. Meneja Pep Guardiola pamoja na mmiliki wa klabu Khaldoon al Mubarak na maafisa wengine wa ngazi za juu wote wamekubaliana katika jambo hilo. Imeripotiwa kuwa mshahara anaodai Sanchez ungemfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi kuliko wachezaji wote nyota wa City, kitu ambacho klabu imeona haiwezi kukifanya.

Post a Comment

 
Top