Simba tayari imempoteza nyota wake Ibrahim Ajibu, ambaye amejiunga na Yanga, huku nao wakitajwa kumsajili kiungo Haruna Niyonzima

Simba imepanga kuivamia tena kambi ya Azam safari hii wakitaka kumchukua mshambuliaji raia wa Ghana, Atta Agyei.

Mratibu wa mabingwa hao wa Kombe la FA, amesema, hivi karibuni alikuwa Ghana na amezungumza na mchezaji huyo ameonyesha kukubali kujiunga na timu yao.

"Tunamuhitaji Atta, kwa sababu ni mchezaji mzuri kwenye nafasi ya ushambuliaji hivyo nimezungumza naye na amesema yupo tayari kucheza Simba," amesema Abbas.

Kiongozi huyo amesema wameamua kumfukuzia mshambuliaji huyo baada ya kuona mambo magumu ya kumsajili mshambuliaji wa AFC Leopards ya Kenya Allan Katerrega.

Amesema wamebakiwa na nafasi moja ya mchezaji kutoka nje watajitahidi kutumia muda uliobaki ili kuhakikisha wanamsajili mchezaji huyo ambye amekuwa chaguo la kwanza kwa kocha Joseph Omog.

Simba tayari imempoteza nyota wake Ibrahim Ajibu, ambaye amejiunga na Yanga, huku nao wakitajwa kumsajili kiungo Haruna Niyonzima ingawa haijawa na uhakika

Post a Comment

 
Top