KOCHA mpya wa timu ya Taifa ya Angola, Roberto Bianchi, amesema kazi kubwa iliyopo mbele yake kwa sasa ni kuirejesha Angola kwenye soka la dunia baada ya kupotea kwa muda.
Bianchi (50) raia wa Brazil amesema kazi kubwa kwake ni kuhakikisha kuwa soka linachezwa kwenye kiwango cha kimataifa na kupata ushindi.
Alisema hilo akifanikiwa hatakuwa na jambo jingine lolote kwenye soka la Angola hasa ikizingatiwa kuwa nchi hiyo ilikuwa ni moja ya mataifa makubwa walioitawala soka la Afrika kwa muda mrefu.
“Angola ilikuwa moja ya timu iliyotawala soka la Afrika kwa muda mrefu kwa maana ilikuwa moja ya timu kubwa iliyoshiriki michuano mikubwa, ila katika siku za karibuni iliweza kupotea,” alisema Bianchi.
Kabla ya kuchukua nafasi hiyo, Bianchi alishafanya kazi kwenye mataifa mbalimbali duniani ikiwemo Jordan, Hispania, Montenegro na Indonesia ambapo sasa anachukua kazi ya Jose Kilamba aliyekuwa anaifanya kazi hiyo tangu mwaka 2015.
Post a Comment