Mkutano wa 71 wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umefunguliwa jana huko New York, ukiwa na kauli mbiu ya "Malengo ya Maendeleo endelevu: Kufanya juhudi za pamoja ili kuboresha dunia yetu."
Akihutubia mkutano huo, mwenyekiti mpya wa mkutano huo Peter Thomson kutoka Fiji amesema, katika kipindi kijacho baraza hilo litaendelea kuchangia katika kuhimiza amani, kupambana na ugaidi, kutatua mgogoro wa wahamiaji, na kupunguza hali mbaya ya kibinadamu, ili kusukuma mbele utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema, mwaka wa kwanza ni muhimu zaidi kwa utekelezaji wa mpango wa maendeleo endelevu, ambapo nchi wanachama wa Umoja huo zinapaswa kutoa misaada ya utungaji wa sera, mipango na fedha kwa ajili ya mpango huo.

Post a Comment

 
Top