Uongozi wa klabu ya Simba unatarajiwa kuwa na kikao na mfanyabiashara Mohamed ‘MO' Dewji’ kesho jijini Dar es Salaam kujadili mpango wake wa kutaka kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. bilioni 20,

zoezi ambalo litailazimu klabu hiyo kwanza kubadilisha katiba ili kuhamia kwenye mfumo wa kuuza hisa.

Kahemela alisema jana kwamba maandalizi yote ya kikao hicho yamekamilika na Kikao hicho kinatarajia kuja na majibu ya mchakato mzima wa kuekelea kwenye mabadiliko.

Katika maombi yake, Mtendaji Mkuu huyo wa Kampuni ya Mohamed Enterprises Tanzania Limited (MeTL), alisema kuwa atakaponunua hisa ailimia 51 atataka kuitoa klabu hiyo kwenye bajeti ya bilioni 1.2 kwa mwaka hadi bilioni 5.5.

Tajiri huyo anaamini kuwa mashabiki wa Simba wanahitaji mafanikio ya haraka, ameahidi kusajili vizuri, kuajiri kocha mzuri, na kuhakikisha Simba inapata mafanikio kimataifa.

Post a Comment

 
Top