Chadema Mnalitakia nini Taifa Hili?
Ndugu zangu mara chache sana mimi kuhoji nia ya siasa zinazofanywa Tanzania hasa ikizingatiwa kuwa mimi napenda sana kuheshimu misimamo ya wengine hasa inayoliunganisha taifa hili.
Wakati Rais Kikwete analiongoza taifa hili kwa miaka kumi Viongozi wa Chadema walipaza mbiu kwamba Jakaya Kikwete ni Rais Dhaifu na mwoga wakaenda mbali wakasema mpaka bungeni serikali ya CCM ni dhaifu na legelege kwamba haichukui hatua na nchi inayumba jambo ambalo kimsingi lilikua ni porojo tuu.
Rais Magufuli ameingia madarakani akija na fikra mpya kabisa ambazo kwetu wazalendo wengi wa hii nchi tulikua tukitamani nchi ipate mtu wa aina hii.Mzee huyu Mzalendo na mnyenyekevu amezima maneno na porojo za Chadema;Waliimba CCM inalea mafisadi na haichukui hatua,Magufuli kwa miezi minne tuu alipoingia madarakani akafanya mambo makubwa yaguatayo.
1.Akadhibiti wizi Bandarini
2.Akafuta watumishi hewa
3.Elimu bure kwa watoto wa Kitanzania na Maskini ikaanza kutokewa
4.Akaongeza mapato ya serikali kwa asilimia karibu 40 zaidi
5.Akadhibiti wakwepaji kodi
6.Akadhibiti nidhamu ya Matumizi ya serikali
7.Akarudisha nidhamu ya uwajibikaji na utumishi kwa Umma.
8.Akafufua shirika la ndege kwa kuagiza ndege mpya kwa pesa zetu ndani ya miezi 7 tuu ya itawala wake.
9.Akatekeleza kwa vitendo serikali kuhamia Dodoma kama zikivyokua ndoto za mwalimu Nyerere
10.Ameendelea kupigania umoja na mshikamano wa nchi huku akileta falsafa ya taifa kujitegemea kiuchumi kwa kuja na Bajeti ya 29 trilioni
Ndugu zangu nimejiuliza Chadema Wanania gani na hii nchi?Demokrasia ni mpaka wao washinde tuu?Mikutano ya kisiasa inaleta maendeleo kwenye nchi chaga kama hii?Wazungu wanaowahadaa walimwengu juu ya demokrasia wao waliyaruhusu haya wakiwa bado wachanga kiuchumi miaka karibu 400 iliyopita?
Chadema mnalazimisha Maandamano mmetumwa na Mungu au na shetani? udikteta wa Magufuli unakomesha wala rushwa;Udikteta unadhibiti matumizi yakipumbavu,udikteta unaonunua ndege za serikali,Udikteta unaodhibiti wabunge kusafiri kutwa ulaya na watumishi wa umma kutwa kushindwa kwenye ndege,Udikteta unaofuta watumishi hewa na kuokoa mabilioni,Udikteta unaozuia maandamano ya kipumbavu ili watanzania wafanye kazi na kuacha siasa za kudanganywa na nchi za magharibi,Udikteta unaotaka watu wapate vipato halali kwa kujituma na kuwa na huruma kwa Maskini wa hii nchi hakika huu ndio udikteta tunautaka.
Chadema acheni utoto;Acheni sifa za kitoto mkidhani siasa ndio iwe agenda ya nchi kila siku.acheni Magufuli atekeleze ahadi za ilani ya CCM mje mkutane naye 2020.Acheni kutumiwa na shetani kuvuruga Misingi kwa uroho wa madaraka.
Mkiupuuza ushauri huu mtaangamia.Nawaambia huyu Magufuli ana kibali cha Mbingu acheni kushindana na Mbingu mtaangamia.Mara nyingi mnadharau mamlaka kwa kisingizio cha demokrasia na maandamano.Maandamano mara nyingi ni kazi ya Ibilisi.Hata kwa Yesu aliwatumia wayahudi kuandamana wakitaka Yesu asulubiwe.
Acheni amani ya nchi kama mlivyoikuta.Kiburi kilimgharimu Shetani akafukuzwa mbinguni.Angalieni nchi msiangalie nafsi zenu na sifa kuwa ninyi ni jeuri.Acheni kuichokoza dola kwenu mna wazee walikua watumishi wa dola waandamizi na wamepata heshima kwa serikali hii hii,Wazee ninyi nawaheshimu sana ila nimeanza kuona mwelekeo wenu hauko upande wa Mungu.
Magufuli hatutakusaliti kwa sabau ndani yako tumeona dhamira imara na ya kwei katika kuwasaidia watu Mungu wa Ibrahimu wa Tafa hili
Chadema acheni kumchokoza Rais Magufuli.
Mungu Ibariki Africa
Mungu Ibariki Tanzania
Post a Comment