KOCHA Mkuu wa Timu ya Gendermerie Nationale, Mvuyekure Issa ameshangaa kufungwa mabao manne tu na Simba SC jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa katika pambano la hatua ya awali ya kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza na waandishi wa Habari baada ya dakika 90 kumalizika, Issa alisema walivyosikia wanakuja kucheza na Simba walijua wangefungwa mabao nane au kumi kwasababu zamani Djibout lilikua suala la kawaida tu kupokea vipigo vikubwa namna hiyo.

“Namshukuru Mungu, kwakweli sikutarajia kufungwa mabao manne tu na Simba, tulitegemea zingekuwa zaidi ya nane au kumi kwasababu zamani ndio ilikuwa kawaida yetu.” alisema.

Post a Comment

 
Top