Ripoti ya kiungo wa simba, Said Ndemla aliyekwenda kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna ya nchini Sweden, inatarajia kuanikwa wiki hii huku maendeleo yake yakionekana kuwavutia wazungu hao.

Ndemla aliondoka nchini mapema Novemba 9, mwaka huu kwaajiri ya majaribio ya siku 14 nchini Sweden baada ya kupata ofa kwenye klabu hiyo ingawa  kwa sasa bado ni mchezaji wa Simba.

Akizungumza na meneja wa kiungo huyo, Jamal Kisongo, alisema taarifa rasmi kuhusiana na mchezaji huyo zinatarajiwa kutolewa mwishoni mwa wiki hii lakini hadi sasa maendeleo yake ni manzuri akiwa amefanikiwa kuwachanganya wazungu kutokana na kiwango chake.

“Tangu amefika kule maendeleo yake kwa ujumla na mazuri kama unavyojua wachenzaji wanapambana kuhakikisha wanafanya vyema lakini repoti yake rasmi itatolewa mwishoni mwa wiki, ndio hatima yake itajulikana.

Baaada ya hili ndemla hilo kukamilika, pia kuna ofa imefika mezani kwangu ya  mchezaji mwingine wakati muafaka ukifika nitawajulisha ni mchezaji gani lakini yote haya ni kuweza kuona vipaji vya wachezaji wetu vinaendelea kukua,” alisema Kisongo.

Post a Comment

 
Top