Kamati ya kuhamasisha watanzania kuichangia timu ya Taifa ya vijana chini ya Umri wa miaka 17 Serengeti Boys imefanikiwa kukusanya zaidi ya Shilingi Millioni 200.
Kiasi hicho cha fedha kimetajwa na Rais wa Shirikisho La Soka Nchini 'TFF' Jamal Malinzi wakati wa Hafla maalum ya Kuichangia Serengeti Boys iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kassim, Ambaye awali alitangaza kufurahishwa na hatua ambayo kamati hiyo imefikia na kuwaomba Watanzania kuendelea kuichangia timu hiyo ili kuiwezesha kufanikisha malengo yao ya kutwaa ubingwa katika Fainali ya Michuano ya Mataifa Barani Afrika kwa Vijana Chini ya Umri wa Miaka 17.
Waziri Mkuu
-Tuna matumaini makubwa na Serengeti Boys Naamini watafanya vizuri tuendelee kuwaunga mkono ili kufanikisha mipango yao, tuna uwezo wa kushinda Mechi zote katika kundi lao, nawasihi tena tuendelee kuwaunga mkono Serengeti Boys, amesema Majaliwa.
Uwazi wa Matumizi.
Aidha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe ameagiza matumizi ya pesa zilizopatikana na zinazoendelea kuchangwa zitumike kwa umakini kwani ni wazi kuwa hizo ni pesa za wananchi.
-Nimefurahi kwa hatua tuliyofikia na tuendelee kuchanga hata kwa wale ambao Bado, nakuhakikishia Waziri Mkuu kuwa utaratibu wa matumizi ya pesa hizo utawekwa wazi kwa wote, pesa hizi ni za wananchi inatakiwa tuzitumie vizuri Ili tuaminike siku nyingine' amesema Mwakyembe.
Viongozi wa mikoa, vilabu na wadau wa michezo pamoja na makampuni na Taasisi mbalimbali ni miongoni mwa
Post a Comment