Kiungo wa Simba ambae amejumuishwa na kikosi cha Tanzania “Taifa Stars”  kinachoshiriki michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini huenda akatimkia nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo figisutz imezipata zinasema vilabu vingine nchini humo vimevutiwa na huduma yake hasa kwa uwezo wake wa kushambulia na kutengeneza mashambulizi.

Mzamiru hadi hivi sasa amecheza kwa ubora wake katika mechi zote ambazo amecheza kwenye michuano hiyo na kuwaduwaza mashabiki na mawakala walioshuhudia mchezo kati ya tanzania Vs Afrika kusini ikishuhudiwa na Tanzania kufuzu hatua ya nusu fainali itakayopigwa kesho.

Post a Comment

 
Top