Gazeti La Habari Leo limeripoti kuwa Klabu ya Simba imepanga kuwaacha nyota wake watatu wa kimataifa kwa utovu wa nidhamu na kushuka kwa viwango vyao. 
Habari Leo imewataja Nyota hao Kuwa ni Jamvier Bokungu raia wa DR Congo na Fredrick Blagnon, mshambuliaji raia wa Ivory Coast wanaodaiwa kushuka viwango.
Wakati Beki Mganda, Juuko Murshi yeye anatemwa kutokana na kudaiwa kukosa nidhamu licha ya uwezo wake uwanjani kuwa mkubwa zaidi.
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Usajili Simba alisema wanawaandalia wachezaji hao barua za kuwataarifu waanze kusaka timu za kujiunga nazo kabla msimu wa usajili haujapita. 
-Kamati yetu imepanga kuachana na wachezaji hao kutokana na usajili tulioufanya, Mfano wa beki wa kulia tumemsajili Shomari Kapombe na Ally Shomari, Hapo Bokungu hana nafasi, Pia kuna mshambuliaji tutamtangaza hivi karibuni kumrithi Blagnon na beki wa kati,” alisema. 
Alisema mbali na nyota hao wa kigeni, pia kuna baadhi ya wachezaji wazawa watawaacha baada ya mchango wao kuwa mdogo klabuni.
Wachezaji hao ni beki wa kulia, Juma Hamad, Pastory Athanas, Jamali Mnyate na Novaty Lufunga walioruhusiwa kutafuta timu msimu ujao na wengine wamemaliza mikataba yao. 
James Kotei. 
Kwa Mujibu wa Habari Leo ni kwamba Simba wapo katika mikakati ya kumwongezea mkataba kiungo wake mkabaji raia wa Ghana, James Kotei ambaye sasa ni mchezaji huru.

Post a Comment

 
Top