Leo katika Matini, tunakuletea maelezo machache lakini yasiyo na upujufu kuhusiana na dini mashuhuri yenye wafuasi wengi duniani, Buddha.

Mpendwa msomaji mwema, wengi tunafahamu ustaarabu wa dini mbili mashuhuri, Ukristu na Uislamu, ambazo zina walei wengi duniani. Inasemekana, kwa mfano, Ukristu una walei/wafuasi wapatao bilioni moja na ushehe ikifuatiwa na Usilamu ambao mpaka sasa sijapata takwimu yake kamili. Bila tashwishwi, wengi tutakubaliana kuwa Ukristu na Uislamu ni ustaarabu ambao umeenea kwa kiasi kikubwa duniani ukilinganisha na staarabu za dini nyinginezo.

Budha, kwa upande wake, bado haifahamiki kindakindaki katika jamii za Kiafrika, hii ni kwa sababu haijaonelea kuathiri mioyo ya watu wengi kama zilivyo dini zilizotajwa hapo awali. Neno “Budha” linatokana na jina la Gautama Buddha. Gautama (563 KK-483 BK) ndiye mwasisi na nembo ya kwanza ya dini ya Budha. Gautama alizaliwa kwenye familia ya Siddhartha katika jiji la Nepal, kusini mwa Asia ya Zamani. Baba yake alikuwa mfalme aliyetwa Suddodana Tharu na mamaye mlimbwende aliyeitwa Mayadevi.

Inadaiwa kuwa kipindi cha uzao wake, Gautama alitabiriwa na mnajimu wa mfalme (baba yake) kuwa Mfalme Mkuu (the Great King), na iwapo angeondoka katika ufalme wake, basi alitakikakana kuwa kiongozi hodari wa dini. Unajimu huu haukumfurahisha babaye ambaye  hakutaka mwanawe awe kiongozi wa dini.

Gautama alipofikia utuuzima na kuelimika vema, alitambua jawabu thabiti la masumbuko/mateso na namna ya kuukabili na kuudhibiti. Jawabu hilo aliliita Four Noble of Truths―suffering (why people unhappy), origin/source, ends (the end of suffering) and marga/means to end the suferring―. Hata hivyo, hakuwa na hakika iwapo atafundisha udhanivu wake huo mpya. Alijiuliza nafsini mwake iwapo ulimwengu utakuwa tayari kupata mafundisho ya namna hii.  Lakini mwishowe, aliamua kusafiri kwenda mjini kuitwapo Sarnath kuwafunza watu njia aliyoimaizi. Alifundisha watu njia hiyo (the eightfold path―the path to the end of suffering), na watu walimakinika kumsikiliza.

Alipokuwa akifundisha, hakujifanyiza kuwa yeye ama ni Mungu na/au hata kuwa mjumbe wa Mungu. Alijitabanaisha kuwa yeye angali binadamu anayetafuta maana ya maisha (enlightenment). Maishaye yote, alitembea kupita mji wa Nepali na sehemu za India akihudumu akihubiria kile alichokuwa akikiamini, na kwamba kila mtu anaweza kutafuta maana ya maisha. Aidha, alianzisha kundi lililoitwa Sangha liliomini katika mafundisho yake. Kwa kweli tupu, watu waliwerevuka kupitia yeye. Na alipofikisha umri wa kipimo cha miaka themanini aliiaga dunia kwa kile kilichodaiwa kuwa alikula chakula chenye sumu (food poison).

Kwa hivi sasa, tangu enzi yake hadi leo, mafundisho ya Gautama Buddha hujulikana kama Buddhism. Buddhism ni namna tu ya kudondoa hisia za  maumivu makali ambayo watu wanahisi ndani ya safu ya mitima yao. Kwa mujibu wa Gautama Buddha, maumivu/mateso ni sehemu ya maisha. Na kwamba, maumivu husababishwa hasa na mrundikano na mshinikizo wa tamaa kali.

Mafundisho ya Buddha yanasisitiza kuwa njia ya kuondoa tamaa na maumivu ni kufanya vitu vyema, kuacha vitu viovu na kufunza akili/ufahamu wa mtu/watu. Aidha, Buddha alifundisha watu kuwa na uwazo/utafakuri yakinifu (meditation), kufikiri kwa kina wakiwa wamekaa kisanskriti.

Pengine haijathibitika, ulimwengu wa ki-Buddha haujasema iwapo Mungu yupo au la. Bali, aghalabu Buddha alifundisha kwamba watu hawapaswi kumtazamia Mungu pekee kutatua mambo yao isipokuwa wao wenyewe. Hii itawezekana pale tu watu wakijifahamu wenyewe (self enlightenment).
Hivi leo, Ubuddha umesambaa sana Asia ambapo mafundisho makuu ni kuhakikisha watu wakiishi katika maisha tulivu na kutawaliwa na ukweli/wema. Maisha tulivu huashiriwa na amani na furaha.

Ni wazi kuwa mafundisho ya Buddha ni murua na yana umuhimu hasa ulimwenguni, na kwamba kila binadamu ana haja ya kupata mafundisho hayo muhimu.
Kwa kufuatilia zaidi mafundisho na undani wa Buddha usiache kupitia vyanzo vifuatavyo: 

http//www.britannica.com/EBchecked/topic/1224840.2010
http//.buddhanet.net/e-learning/Buddhism/disciples 13.2010.

 Image result for buddha imagesImage result for buddha images







Post a Comment

 
Top