Ligi Kuu ya Uiengereza (EPL) imeendelea hapo jana ambapo mechi iliyoangaziwa kwa hamu kubwa kati ya Spurs (ya Jijini London) ikimenyana vikali na Manchester City katika dimba la White Hart Lane, ikimalizika kwa Wenyeji Spurs kuondoka na ushindi mnono wa 2-0; ushindi uliomwanchia majonzi mkufunzi machachari wa Man City, Pep Guardiola ambaye alikuwa hajafungwa mechi sita za Ligi Kuu. Magoli yote yalifungwa kipindi cha kwanza na Aleksandar Kolarov (aliyejifunga dakika ya tisa ya mchezo) na Delle Alli dakika ya 37. Kwa mujibu wa beki wa zamani wa Manchester United na mchambuzi wa michezo katika Kituo cha Runinga cha Sky sports, Garry Neville, kiongo mahiri wa Spurs mwenye asili ya nchi ya Kenya Victor Wanyama ndiye mchezaji bora wa mechi. Neville alimlimbikizia sifa kiungo huyo kwa kuweza kuutawala mchezo vema. Licha ya kiungo mshambuliaji wa Spurs, Lamela kukosa penati kipindi cha pili, Spurs ilicheza katika kiwango hali ya juu.
Mechi nyingine zilizochezwa hapo jana ni pamoja na:
Man United vs Stoke city 1-1
Burnley vs Arsenal 0-1
Leicester City vs Southampton 0-0
Post a Comment