Klabu inayoshiriki ligi kuu uingereza, Swansea City (ya Wales), imemfuta kazi aliyekuwa mkufunzi wa klabu hiyo, mtaliano, Francesco Guidolin, na kumwajiri kwa muda kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani Kasikazini, Bob Bradley. Guidolin ambaye alikuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa (zaliko), alifutwa kazi tarehe 3 Oktoba, (siku ya Jumatatu), baada ya kufungwa 2-1 na Liverpool siku ya Jumamosi. Swansea imeshinda mechi moja  tu ya kufungua ligi kati ya saba ilizocheza msimu huu. Licha ya kuiokoa timu hiyo kutoshuka daraja, mkufunzi huyo aliandikiwa barua ya kukatishwa kandarasi yake, leo Jumatatu. Mkufunzi huyo alijiunga na klabu hiyo Januari mwaka huu kwa kandarasi (contract) ya miaka miwili.

Post a Comment

 
Top