Balague hakubaliani na maneno ya Zidane kuwa sababu ya matokea mabovu ya michezo minne ya hivi karibuni, ni kukosekana kwa viungo wawili majeruhi Casemiro na Mondric. Anadai kuwa kukosekana kwa wachezaji wawili haimaanishi ufungwe na timu ndogo kama Eibar. Isitoshe, uwanjani, wachezaji wa R. Madrid wameonesha viwango vya chini, na pia, timu haioneshi ufundi wowote uwanjani na haiujui inafanya nini. Hii inatia mashaka mafunzo (training) wanayopata wachezaji kutoka kwa kocha wao.
Kwa upande wa mahasimu wao, A. Madridi wameendelea kutaka baada ya kuwafunga Valencia 2-0 na kuwahakikishia kuongoza msimamo wa ligi.



Post a Comment