Akihutubia katika kongamano (event) katika Chuo Kikuu cha Bogota's Sergio Arboleda, rais wa FIFA, mwitaliano Gianni Infatino, amesema (pendekezo) kuwa mashindano yajayo ya Kombe la Dunia yatashirikisha timu 48. Akielezea udhanivu (idea) wake huo mpya, amedai kuwa timu shiriki zitaanza na mchezo mmoja wa mtoano ambapo timu 16 zitatolewa, na 32 zitakazosalia ndizo zitakazoingia katika hatua ya makundi. Hata hivyo, amesema kuwa maamuzi ya kuthibitisha ushiriki huo mpya utaamuliwa mnamo mwaka 2017, mwaka mmoja kabla ya kuanza mashindano hayo yenye washabiki wengi duniani.

Infatino aliteuliwa na FIFA 26 Februari, mwaka huu kukaimu nafasi ya Sepp Blatter, ambaye alifungiwa miaka sita kwa makosa ya kimaadili.



Gianni Infantino

Post a Comment

 
Top