PAMOJA na Simba kufanya usajili wa nyota wengi bado jukumu la kuziba pengo la kuondoka kwa mshambuliaji Ibrahimu Ajibu aliyetimukia Yanga limeachwa kwa Mohammed Ibrahim.

Hiyo ilikuwa ni kauli ya winga wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe alisema; “Ibrahim anaweza kuwa mchezaji sahihi ambaye anaweza kucheza nafasi hiyo kwa uwezo na ufanisi mkubwa tena zaidi ya alivyokuwa anafanya Ajibu, na akaisaidia Simba kupata matokeo ya ushindi.”

Beki kisiki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa alisema; “Simba wana wachezaji kama Mohammed Ibrahim na Said Ndemla, kama wakipata nafasi na kuaminiwa kwa kiasi kikubwa wana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo na wakafanya kazi vizuri ambayo ni zaidi iliyokuwa ikifanywa hapo awali.”

Pawasa alisema kuwa alitamani kumuona Ajibu anakwenda kucheza soka nje ya nchi kama alivyokuwa akitakiwa katika nchi ya Misri na Afrika Kusini na si kubaki hapa nchi kama alivyoamua kusaini Yanga

Post a Comment

 
Top