1.LIVERPOOL imeanza mchakato wa kutaka kumsajili Winga wa Sporting Lisbon Mreno, Gelson Martins ambaye inaelezwa ana thamani ya pauni £52m. (#Association_Sport)·
2.REAL MADRID inataka kumuweka sokoni Fowadi wake Cristiano Ronaldo huku wakisema kuwa kwa klabu inayomtaka itabidi itoe pauni €180m ambapo vilabu vya Man United, Monaco na PSG vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo ambaye pia anatakiwa na vilabu vya China. (#A_Bola)·
3.HECTOR BELLERIN wa Arsenal anailazimisha klabu yake imuuze kwenda Barcelona baada ya tetesi kuzagaa kuwa anatakiwa na miamba hiyo ya hispania. Imeelezwa kuwa Beki huyo ameshakubaliana na Barcelona kilichobaki ni klabu yake kutaja dau wanalolitaka. Hata hivyo inaelezwa kuwa atapatikana kwa dau la pauni £43m. (#El_Mundo_Deportivo)·
4.LIVERPOOL imeulizia upatikanaji wa James Rodriguez wa Real Madrid ili waweze kumsajili. Wababe hao wa Anfield wameweka £52m mezani kwa nyota huyo wa Colombia. (#Don_Balon)·
5.KOCHA wa Juventus Massimiliano Allegri amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na Juventus utakaoisha mwaka 2020. (#ESPN_FC)·
6.ARSENE WENGER atatumia pesa alizopewa na Uongozi wa klabu hiyo ili kumsajili Fowadi wa Lyon, Alexander Lacazette. (#The_Sun)·
7.BOURNEMOUTH inataka kumsajili beki mkongwe wa Chelsea , John Terry. (#Sun)·
8.CHELSEA & MAN UNITED zimehusishwa katika mpango wa kutaka kumsajili Kiungo Mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala. (#Mundo_Deportivo)·
9.RAIS wa Torino Urbano Cairo ameiambia Manchester United kuwa kama inamtaka fowadi wake Andrea Belotti itabidi itoe pauni £100m. (#Gazetta_dello_Sports)·
10.KOCHA Antonio Conte wa Chelsea bado anafanya harakati za kutaka kumsajili fowadi wa Everton, Romelu Lukaku. (#Evening_Standard)·
11.SOUTHAMPTON inataka kumuajiri kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel. (#Sun)·
12.JUVENTUS inataka kumsajili kiungo wa Chelsea Nemanja Matic. (#Italy)·
NAWATAKIA SIKU NJEMA!!!!
Post a Comment