Cristiano Ronaldo ameweka rekodi, Real Madrid imeweka rekodi, na Super Cup itakuwa ni Madrid dhidi ya Manchester United

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amesema kuwa timu yake imonyesha kwa mfano ni kwa nini wao ni timu "Bora" Ulaya.

Mreno huyo ameingia kwenye ubao wa magoli mara mbili Madrid wakiifagia pembeni Juventus kwa kipigo cha mabao 4-1 mjini Cardiff kushinda mara mbili mfululizo taji la Ligi ya Mabingwa, na rekodi ya mara 12 katika taji hilo la Ulaya.

Kwa Ronaldo kupitia mchango wake usiku huu, ametimiza magoli 600 na amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye fainali tatu za Ligi ya Mabingwa.

"Tumekuwa timu ya kwanza kushinda Ligi ya Mabingwa miaka miwili mfululizo, nimefunga magoli mawili katika fainali na nimekuwa kinara wa mabao katika michuano ya msimu huu, kwa hiyo nina furaha," Ronaldo alikiambia beIN Sport.

"Ni rekodi nyingine kwetu, na tumestahili. Lengo sasa ni kushinda michuano ijayo ya Ligi ya Mabingwa kama tulivyoshinda hii, kuonyesha kwamba sisi ni timu bora na tunatumia vizuri nafasi kwani tumeonyesha hili tangu mwanzo.

"Nilijiandaa kwa ajili ya hili, na tulijua kwamba mataji makubwa hupatikana mwisho. Zinedine Zidane alizungumza nasi vizuri na kutupa imani. Anajua kwamba kikosi chake ni kizuri sana, na tumedhihirisha ubora wetu. Umekuwa mwisho mzuri wa msimu."

Real Madrid sasa watakabiliana na mabingwa wa Ligi ya Europa Manchester United kuwania Super Cup Jumanne ya

Post a Comment

 
Top