Aishi Manula ameungana na John Bocco kutua Msimbazi rasmi kujiunga na Simba ingawa amesema hataki kulizungumzia sana hilo kwa sasa

Klabu ya Simba imefanikiwa kuinasa saini ya kipa namba moja wa Azam Aishi Manula, aliyesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo.

Manula ameiambia figisutz, tayari amejiunga na timu hiyo kwa dau la milioni 60, na hiyo inatokana na Azam kutokuwa na nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.

“Ni kweli nimesaini Simba lakini nisingependa sana kuongelea jambo hili, kwa sababu bado ninamkataba na Azam ambao unamalizika June 30 mwaka huu,” amesema Manula.

Kipa huyo amesema ameamua kuachana na Azam kwa sababu mbalimbali mojawapo ni hiyo ya kushiriki michuano ya kimataifa ambayo kwake ni kitu kikubwa.

Amesema hata klabu ya Singida United ilimuhitaji lakini alishindwa kujiunga nayo kwa sababu ni timu mpya na haina nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa kama ilivyosimba

Kipa huyo ambaye pia anaichezea timu ya taifa amesema ameamua kutua msimbazi ili kuungana na nahodha wake John Bocco, ambaye naye amehamia timu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake.

Azam inatarajiwa kuondokewa na wachezaji wengi kutokana na matatizo mengi yaliyoikumba klabu hiyo kiasi cha kumtimua hata Mtendaji mkuu wao Saad

Post a Comment

 
Top