PAMOJA na ushindi wa bao moja walioupata timu Yanga dhidi ya MC Alger kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika uliofanyika katika uwanja wa Taifa bado mabingwa hao wa Tanzania bado wana kazi kubwa ya kufanya ili kufuzu kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Yanga walionyesha mapungufu kwenye idara ya ulinzi hasa kipindi cha pili kwa kukosa umakini ambapo wenyeji kama wangefanya mashambulizi ya haraka wangeweza kuleta madhara langoni mwao.

Yanga walianza mchezo huo kwa kasi kwa kufika mara nyingi zaidi langoni mwa Alger lakini ubutu wa safu ya ushambuliaji ulipelekea timu hiyo kwenda mapumziko bila bao kwani Obrey Chirwa na Thaban Kamusoko wakikosa nafasi mbili za wazi kila mmoja.

Wageni walicheza kwa utulivu mkubwa hasa safu ya ulinzi kuhakikisha hawaruhusu bao la mapema ambalo lingewatoa mchezoni huku wakiwa hawajafanya shambulizi lolote la hatari langoni mwa Yanga katika kipindi cha kwanza.

Kamusoko aliipatia Yanga bao hilo pekee dakika ya 60 kufuatia pasi safi kutoka kwa Chirwa baada ya kupigiana pasi murua ndani ya eneo la 18 la Alger.

Baada ya bao hilo Alger walifanya mashambulizi machache lakini Yanga waliendelea kutengeneza nafasi na kufanya mashambulizi tatizo likabaki kwenye umaliziaji.

Kocha wa Alger Moussa Kamel aliwatoa Goveri Kaled, Nekkache Hichem na Bougueche Hajj na kuwaingiza Seguer Mohammed, Awady Said pamoja na Feedab Zahir.

Kwa upande wa kocha George Lwandamina wa Yanga aliwaingiza Donald Ngoma na Emmanuel Martin kuchukua nafasi za Deus Kaseke na Haruna Niyonzima.

Mchezo wa mkondo wa pili utafanyika nchini Algeria Aprili 16.

Post a Comment

 
Top