KITENDO cha mabeki wa kati ya Yanga, nahodha Nadir Haroub  ‘Cannavaro’ na Vicent Bussou kuingia kimiani hivi karibuni mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni kama wamemshtua winga wa Simba, Shiza Kichuya, aliyedorora kufunga.

Bossou na Cannavaro mwishoni mwa wiki iliyopita wawili hao walifanikiwa kufunga mabao katika michezo miwili tofauti kwa mabao ya vichwa, tofauti na Kichuya ambaye hajaingia wavuni tangu mzunguko wa pili wa Ligi Kuu uanze.

Cannavaro aliifungia timu yake hiyo dhidi ya Stand United katika ushindi wa mabao 4-0, kama ilivyokuwa kwa beki mwenzake, Bussou mbele ya Ndanda.

Nyota hao ni wachezaji pekee wanaocheza safu ya ulinzi kwenye vikosi hivyo kuingia kimiani  ndani ya mzunguko huu wa pili wa ligi hiyo.

Post a Comment

 
Top