Msanii wa Jahazi Morden Taarabu Amingo Prince amesema baada ya maamuuzi ya Mzee Yusuph kuachana na muziki na kumrudia Mungu wasanii 15 akiwemo Khadija Yusuph wameihama bendi.

 

Akipiga story ndani ya eNews Amigo amesema baada ya Mzee kuacha muziki wasanii walianza kuyumba kiuchumi na baadhi ya wasanii kuona maisha yao yatakuwa magumu na kuanza kuhama  mpaka sasa wamebaki wasanii 4 kwenye bendi ya Jahazi.

Pia Amigo amesema bendi ya Jahazi ilikuwa chini ya Hamisi Doa baada ya Mzee kuondoka  lakini pia hata Khadija Yusuph alipewa kipaumbele cha kutosha na alikuwa akishirikishwa katika vitu vingi katika bendi hiyo anashangaa ni kwa nini aliamua kuondoka na kuwaacha

Post a Comment

 
Top