Klabu ya Simba itafanya mkutano mkuu wa wanachama Disemba 3 kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mabingwa hao wa kombe la FA.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano ya klabu hiyo Hajji Manara inasema ajenda za mkutano huo zitatolewa siku chache zijazo.

Simba inaendelea na mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa kiundeshaji wa klabu hiyo kwa njia ya hisa ulianza miezi kadhaa iliyopita.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

 
Top