Klabu ya simba imeiandikia barua wizara yenye dhamana na michezo kulalamikia waamuzi wa mchezo uliofanyika katika uwanja wa uhuru juamosi ikidai kutokana na makosa ya kimaamuzi yaliyopelekea timu hiyo kuambulia sare katika mchezo wao dhidi ya mahasimu wao yanga.
Akizungumza na wanahabari msemaji wa timu hiyo haji sande manara amesema mbali na kuiandikia barua wizara ya habri utamaduni sanaa na michezo pia wameiandikia barua shirikisho la mpira wa miguu nchini tff na nyingine kuielekeza kwa bodi ya ligi.
Akitumia mkanda wa video kuonyesha makosa yaliyofanywa na waamuzi katika mechi tatu tofauti za ligi kuu ikiwemo pambano kati ya simba na yanga, na mchezo wao dhidi ya stendi na mbao ni mwendelezo wa vitendo vya waamuzi vinavyoonyesha mazingira ya kuiminya timu ya simba husasan pale wanapokutana na mahasimu wao.
Aidha bwana haji manara amesema hali ya ufinyu wa uwanja wa uhuru imepelekea kukosekana kwa mashabiki wengi kama ilivyozoeleka.
Akijibu hoja hoja za wachambuzi na zinazotolewa katika mitandao ya kijamii, manara amesema anawashangaa wale wanaoibeza simba kwa kutoka sare ikilinganishwa na kikosi cha timu yanga.
Wekundu wa msimbazi simba imeanza mazoezi hapo jana ikiwa na wachezaji wake wote na wanatarajia kusafiri kuelekea jijini mbeya siku ya ijumaa tayari kwa kujiandaa kuvaana na timu ya mbeya city.
Post a Comment