Kiungo wa mchezeshaji wa klabu ya Mtibwa Sugar, Mohammed Issa 'Banka' amesema yuko tayari kukipiga Simba au Yanga

Banka amekuwa muhimili mkubwa kwenye kikosi cha Mtibwa Sugar kwa msimu huu, kwa kuifanya klabu hiyo kuwa moja ya timu zenye safu bora ya kiungo.

Uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi fupi fupi na ndefu,  kuchezesha timu, na kukaba pindi timu ikipoteza mipira ndiyo sababu kubwa ya mashabiki kumfananisha na kiungo wa zamani aliyewahi kuzichezea klabu za Simba na Yanga, Mohammed Bank.

Akihojiwa Mohammed Issa amesema yuko tayari kuhamia Simba au Yanga kwenye dirisha dogo la usajili, kama wakikidhi mahitaji yake tu maana yeye mpira ndiyo kazi yake.

“Nahitaji kufika mbali katika maisha yangu ya soka ikiwezekana kujituma ipasavyo kuweza kufanikiwa kama ilivyo kwa Mbwana Samatta.

“Iwapo Simba na Yanga zitanihitaji kunisajili nitakuwa tayari kuzichezea kwa kuwa moja ya malengo yangu ni kufanikiwa katika soka na hata kuichezea timu mojawapo kati ya hizo,” alisema Banka.
Source salehe jembe

Post a Comment

 
Top