Kiungo wa kimataifa wa Simba Haruna Niyinzima, ameitabiria pointi tatu timu yake licha ya ubora wa kikosi cha wapinzani wao Yanga
Kiungo wakimataifa wa Simba, Haruna Niyonzima amesema mchezo wa Jumamosi hautakuwa rahisi kwao kutokana na ubora wa timu hizo kulingana.
Niyonzima aliyewahi kutamba na Yanga kabla ya kujiunga na Simba msimu huu amesema kinachofanya mchezo huo kuwa mgumi ni upinzani uliopo baina ya timu hizo mbili na kingine ni presha ya ubingwa ambayo timu zote mbili inazikabili.
"Ujue mechi hii ndiyo inaonyesha mwelekeo wa bingwa wa msimu husika ndiyo maana ukiacha upinzani kila upande unacheza kwa tahadhari kuhofia kutofungwa na kujiweka katika mazingira mazuri ya ubingwa," amesema Niyonzima.
Niyonzima amesema yeye binafsi siku hio amepanga kuwavalia Yanga miwani ya mbao na kuipigania timu yake ya simba kutwaa taji hilo kwa Mara ya kwanza baada ya misimu minne kupita bila taji la michuano hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Post a Comment