Klabu ya Yanga imekuwa na mahusiano mazuri na Mbeya City kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kuchukua baadhi ya watendaji wao mara kwa mara

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro amewataka wapenzi na mashabiki wa Jangwani kumuunga mkoni msemaji wao mpya aliyetokea klabu ya Mbeya City ya Jijiji Mbeya , bwana Dismas Ten 

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Jerry Muro ameunga mkono  uteuzi wa ya Yanga kwa kumteua Dismas Ten kuwa msemaji wao mpya akichukua nafasi ya Godlisten Anderson "Chicharito" ambaye alikuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda kutokana na aliyekuwa msemaji, Jerry Muro kufungiwa mwaka mzima na chama cha mpira Tanzania (TFF)

"Breaking News. Hatimae Club ya @yangasc imemtangaza Msemaji Mpya wa Club Bw Dismas Ten, Naunga mkono uteuzi wake, Naomba wana @yanga_sc_fans wote tumuunge mkono Dismas Ten aweze kutimiza wajibu wake, KARIBU YANGA" alisema hivyo Jerry Muro

Jerry Muro alifungiwa mwaka mzima na chama cha soka Tanzania kutojihusisha na mpira kutokana na kupatikana na makosa matatu yaliyokuwa yanamkabili , makosa yaliyomtia hatiani Muro ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 5 baada ya kufanya makosa, lakini amekaidi kulipa hadi leo. Kwa kosa hilo akahukumiwa kutengana na masuala ya soka kwa mwaka mmoja .

Shitaka lingine lililomtia hatiani ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC amabao Wanajangwani walipoteza mchezo huu wa goli moja kwa

Post a Comment

 
Top