Taifa Stars walifika hatua hiyo ya Robo Fainali baada ya kuongoza kundi A la michuano hiyo kwa kuwa na Alama 5 na kuwaacha Angola, Mauritius na Malawi wakiaga mashindano hayo wakati Afrika Kusini wao walitinga Moja kwa Moja katika Hatua hiyo.
Dakika 90.
Mpira Ulianza kwa kasi ambapo dakika ya Sita Afrika kusini walilisogelea lango la Stars na Kupiga Shuti kali kupitia kwa Lehlogonolo Masalesa laiki Mlinda mlango Aishi Manula akapangua na kuwa kona ambayo ilipopigwa haikuzaa matunda.
Mshikemshike huo uliwafanya Tanzania Kutulia na kuanza kucheza Soka la Kuelewekwa la Pasi fupifupi na za haraka ambazo zilizaa Matunda ambapo dakika ya 17 Mshambuliaji Elias Maguli akaiweka Tanzania Mbele baada ya kufunga bao Safi akipewa pasi Murua na Kiungo Mzamiru Yasini.
Baada ya bao Hilo Kila Timu ikaanza kucheza mchezo wa kujihami zaidi hali iliyopoteza radha ya mchezo huo kwani hadi Timu zinakwenda mapumziko Tanzania walikuwa wakiongoza kwa bao Hilo moja dhidi ya Afrika Kusini.
Kipindi cha Pili Tanzania Waliingia wakiwa tofauti kwani dakika Nne tu baada ya kutoka Vyumbani Kocha Salumu Mayanga alifanya Mabadiliko ya kiufundi katika eneo la Ushambuliaji kwa Kumtoa Thomas Ulimwengu na Kumuingiza Simon Msuva mabadiliko ambayo kwa kiasi Fulani yaliongeza nguvu eneo hilo.
Kuingia kwa Simon Msuva pia kuliongeza uhai wa eneo la Kiungo kwani Mzamiru Yasin na Raphael Daudi walicheza kwa uhuru zaidi na kumfanya mlinzi wa Pembeni Gadiel Michael kupanda zaidi mbele ambapo dakika ya 66 alipiga Krosi ambayo ilikosa mmaliziaji na kutoka Njee.
Katika dakika ya 86 Mlinda Mlango Aish Manula alipewa kadi ya Njano kwa kosa la kupoteza muda, lakini pia zilipoongezwa dakika Kocha Salumu Mayanga aliwaingiza Viungo Salmin Hoza na Hamimu Aboubakar Tamimu kuchukua nafasi za Raphael Daudi na Shizya Kichuya.
Hadi Kipyenga cha Mwamuzi wa Mchezo huo kinapulizwa Tanzania Moja na Afrika Kusini Sifuri na kuwafanya Tanzania Kufuzu moja kwa moja hatua ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo itakayofikia tamati Julai 9 Mwaka huu.
Nusu Fainali.
Ratiba inaonesha Tanzania watacheza na Zambia katika Hatua ya Nusu Fainali Julai 5, Katika Uwanja wa Moruleng, Mchezo unaotarajiwa kuanza majira ya Saa 12 Jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Post a Comment

 
Top