Timu ya Soka ya AJAX imethibitisha kwamba Mchezaji wake kinda Abdelhak Nouri "Appie" aliyeanguka uwanjani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Weder Bremen amepata Matatizo ya Kudumu katika Ubongo na nafasi ya kupona na kurejea uwanjani ni "Nill" (0).
Nouri mwenye Miaka 20 na kipaji cha hali ya juu amekuwa akitarajiwa kuwa Nyota wa Uholanzi kwa siku za Usoni lakini inavyoonekana ndoto za Kijana huyu,Ajax na Uholanzi zimefika Ukomo, its terrible, ni Mungu pekee awezae kumponya,
Vipimo vya MRI kwenye Ubongo vinaonyesha kwamba ubongo wake haufanyi kazi kwa kukosekana kwa Oxygen Supply, na kabla ya kuanguka uwanjani katika dk ya 70 alipata mashambulio kadhaa ya Moyo, baada ya kupata matibabu ya awali amerejeshwa Uholanzi, kwa sasa hawezi kuongea,kula, kutembea wala kufanya chochote, Madaktari wanasema hatopona.
Ashindwacho Binadamu Mungu hashindwi, Mungu na akasimame katikati yake na Familia yake kuwapa Tumaini na hata kumponya: Amen.
Source.soka
Post a Comment