Kiungo Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda Emmanuel Arnold Okwi amewasili usiku huu katika Uwanja wa kimataifa wa mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitoka kwao nchini Uganda.
Hii ni mara ya tatu Okwi kurudi Simba baada ya Kuuzwa katika Klabu ya Denmark
Makamu wa rais wa klabu ya Simba Godfrey Nyange Kaburu alikuwepo katika uwanja Wa Ndege kumpokea Okwi
Okwi atakuwa na mazungumzo ya mwisho na Uongozi kabla ya kusaini kandarasi ya Miaka Miwili kuitumikia tena Simba katika Msimu wa 2017-2018
Post a Comment