Shirikisho la Soka Tanzania TFF juzi May 17 2017 kupitia tovuti rasmi ya shirikisho hilo imetangaza majina matano ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 na watapigiwa kura hadi May 23 saa 6:00 usiku.

Majina ya wachezaji watano yaliyotajwa na shirikisho la soka Tanzania TFF niHaruna Niyonzima wa YangaSimon Msuva wa YangaAishi Manula wa Azam FC, Shiza Kichuya wa Simba na Mohamed Hussein Tshabalala wa Simba.

Utoaji wa tuzo hizo utafanyika May 25 2017 lakini mshindi wa tuzo hiyo atapatikana kwa kupigiwa kura na makocha wakuu na wasaidizi wa vilabu vya Ligi Kuu Tanzania bara pamoja na wahariri wa habari za michezo ambapo watatumiwa fomu maalum za kupiga kura.

Post a Comment

 
Top