Nahodha wa timu ya Taifa ya Vijana Chini ya Umri wa Miaka 17 'Serengeti Boys' ,Dickson Nickson Job ndiye aliyeteuliwa Mchezaji bora (Man of thé Match) katika mchezo wa pili wa Kundi B ambao ulizikutanisha timu ya Tanzania na Angola Katika mchezo ambao umefanyika Jumatano Libreville, Gabon.
Tanzania ambao walionyesha mchezo mzuri dakika zote 90 wakionekana kumiliki mpira waliwafunga Angola kwa mabao mawili kwa moja katika mchezo huo ambapo Kiungo huyo alionyesha kiwango kizuri.
Mchezaji Bora
Job ambaye ameteuliwa na jopo la makocha ambalo limesimamiwa na Afisa Habari wa Shirikisho La Soka Duniani (Fifa ), Ahmed Hussein ,Huameelezea kuwa Jopo hilo limeafikia hatua hiyo baada ya kuridhishwa na mchango wake ulioipelekea Serengeti Boys kupata ushindi wa mabao 2-1.
Nafasi ya pili
Tanzania ambao wako kundi B wakishika nafasi ya pili watacheza dhidi ya Niger katika mchezo wa mwisho wa makundi wakati Mali wakicheza dhidi ya Angola.
Post a Comment