Rufaa iliyokatwa na klabu ya Simba kupinga maamuzi ya kamati ya Sheria, Hadhi na haki za wachezaji imekataliwa na Shirikisho la Soka Duniani, FIFA.
Kwa mujibu wa barua kutoka FIFA, maamuzi ya Kamati ya TFF yatabaki vilevile hivyo kumaanisha Kagera kuendelea kubaki na pointi zao walizoshinda uwanjani kwa kuifunga Simba.
Matumaini pekee ya Simba ni kuamua kukata rufaa katika mahakama ya usuluhishi wa michezo (CAS).
Mtandao wetu wa figisutz, unaendelea na jitihada za kufahamu uhalali wa nyaraka hio ya FIFA kwa kuwa kujaribu kuwasiliana na viongozi wa Simba na TFF mara baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho.
Post a Comment