Leo kwenye U-Heard ya XXL ya Clouds FM Soudy Brown ametuibia mazungumzo aliyokuwa akizungumza na mmoja kati ya maproducer wakali hapa nchini Mesen Selekta, akipokea malalamiko kutoka kwa producer huyo kuhusiana na interview aliyofanya siku chache zilizopita na msichana anayesemekana kuwa amezaa na producer huyo.
Malalamiko ambayo yalidai kurudishwa kwa barua ambayo producer huyo aliipeleka kwenye familia moja kwa nia ya kuchumbia.
Pia Soudy Brown amepiga story na msichana huyo ambaye anadai kujifungua mtoto wa Mesen Selekta na kutaka kujua ni uamuzi gani atauchukua endapo Mesen anataka kuoa mwanamke mwingine.
Uhondo kamili nimekuwekea kwenye video hii hapa chini. Bonyeza play kusikiliza mwanzo hadi mwisho.
Post a Comment