Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema anakiandaa kikosi chake vizuri ili kuhakikisha kinafanya vizuri katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe utakaopigwa Novemba 13 mwaka huu.
Mkwasa amesema, wachezaji wa kimataifa pia wameshawasili kambini ambao ni Elias Maguli, Mbwana Samatta pamoja na Thomas Ulimwengu ambaye ni mchezaji huru.
Kikosi cha Stars kinatarajiwa kuondoka leo jioni kuelekea nchini Zimbabwe ambapo kabla ya safari yao, asubuhi ya leo kikosi hicho chenye wachezaji 23 mpaka sasa, mara baada ya Mwantika kuwa majeruhi kitafanya mazoezi ambapo kocha atachagua wachezaji 20 anaotakiwa kuondoka nao kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa mwishoni mwa wiki hii.

Post a Comment

 
Top