Hivi karimuni moja kati ya vitu ambavyo vilitrend kinoma noma katika mitandao ya kijamii ni pamoja na hashtag ya Ommy Dimpoz katika post yake ya Instagram iliyosomeka kama #WeDontBuyviews, Hashtag ambayo ilichukuliwa kama kijembe kwa msanii mwenzake Diamond Platnumz kuhusishwa na tuhuma za kununua views katika mtandao wa Youtube.
Jana kwenye XXL Ommy Dimpoz alikuwa na exclusive interview akizungumzia mengi kuhusu muziki wake pamoja na matatizo ambayo wanayo na msanii mwenzake Diamond Platnumz.
Moja kati ya vitu ambavyo alivizungumzia Ommy Dimpoz ni pamoja na hashtag yake hiyo ya #WeDontBuyviews akidai kuwa yeye aliandika hivyo pasipo na kumlenga mtu wala nini lakini alikuwa anahitaji kutoa elimu kwa umma kwamba kuna uwezekano wa kununua views katika mtandao wa Youtube.
“Mimi siku mmention mtu lakini niliongea tu kuwa sasa hivi mtu unaweza kununua views, lakini sio kitu kizuri kwa msanii kwasababu unakuwa unajidanganya, yani unajitekenya halafu unacheka mwenyewe.’
Kiufupi tu hayo ni maneno machache mno kati ya mengi ambayo Ommy Dimpoz alifunguka wakati akitolea ufafanuzi issue hiyo ya views. Cha msingi ni kuplay hii video hapa chini ili kusikiliza akifunguka mwanzo hadi mwishO
https://youtu.be/ZM6eBpQYKJs

Post a Comment

 
Top