Sheria tata za mtindo wa nywele yazua gumzo Afrika Kusini

Sheria ambayo imechukulia kama ubaguzi wa raingi nchini Afrika Kusini katika shule za upili yazau gumzo nchini humo.

Sheria hiyo kwa wanafunzi wa kike ilitolewa kwa wanafunzi  kuwa wanatakiwa kulainisha nywele zao.

Bada ya sheria hiyo kutolewa wanafunzi waliingia mabarabarani kupinga sheria hiyo kote nchini.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari Afrika Kusini ni kwamba sheria hiyo katika shule Pretoria imekemewa vikali na kuzua gumzo.

Wanafunzi wa kike wamafahamisha kuwa walimu zao huwapa kero wakiwataka kulainisha nywele zao huku wakiwakataza kuchana mtindo wa Afro ambao nywele huoa katika hali yake ya asili.

Maandamano ya kupinga sheria hiyo yalifanyika mbele ya moja ya shule  Pretoria.

Hatua hiyo imekemewa katika mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake waziri wa utamaduni wa Afrika Kusini  Nathi Mthethwa katika ukurasa wake wa Twitter amafahamisha kuwa ni wajibu wa shule kuwafanya wanafunzi kuweka pembeni tofauti zao na kuwaweka pamoja katika hal ina harakati za mshikamano na ushirikiano.

Post a Comment

 
Top