Ushindi wa bao moja ulioupata timu ya Simba dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Sokoine jioni ya leo umeirejesha kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha pointi 19.
Kabla ya mchezo huo Azam ilikuwa ndiyo kinara ikiwa na pointi 19 kufuatia ushindi wa bao moja uliopata jana mbele ya Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Azam complex lakini Simba wamepanda kileleni baada ya kuwa na uwiano mzuri wa mabao.
Bao hilo pekee la Simba likifungwa na winga Shiza Kichuya dakika ya saba baada ya mabeki wa City kuweka mtego wa kuotea katika mpira uliopigwa na Jonas Mkude.
Simba ilicheza vizuri zaidi kipindi cha kwanza kwa kuliandama lango la City na kumiliki mpira lakini hawakuweza kupata bao la kuongeza.
Kipindi cha pili wenyeji walirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Simba lakini safu ya ulinzi iliyokuwa chini ya Juuko Murshid na James Kotei ilikuwa imara kumlinda Aishi Manula.
Simba itaendelea kubaki nyanda za juu kusini kwani baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa wikiendi ijayo ratiba inaonyesha inatakiwa kucheza na Tanzania Prisons katika uwanja huo huo wa Sokoine.
Matokeo Mengine
Lipuli 1-1 Mwadui
Post a Comment