KATIKA hali ya kushangaza nyota wapya wa klabu ya Simba Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi hawakuwepo miongoni mwa wachezaji waliowasili kutoka nchini Afrika Kusini walipoweka kambi ya wiki tatu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi huku taarifa za ujio wao zikijaa sintofahamu.

Wachezaji wa Simba walisafiri kwa awamu tatu ambapo kundi la kwanza lililokuwa na wachezaji sita liliwasili saa 7 mchana wakati la pili likiingia saa 8 usiku likiwa na nyota saba na la mwisho likiwasili saa tisa usiku likiwa na wachezaji sita.

Kamera ya yetu ambayo iliweka kambi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA)  haikufanikiwa kuwaona nyota hao huku taarifa zenye mkanganyiko zikitoka ikiwemo kuwa wamefichwa ili watambulishwe kwenye tamasha la Simba Day Agosti 8.

Hili ndilo kundi la mwisho lililotua majira ya saa 8 usiku. Katika kundi walikuwemo pia nyota Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Mohamed Ibrahim, Jamal Mwambeleko na Laudit Mavugo

Mwanzoni mwa wiki mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa timu ya Simba, Haji Manara alithibitisha mbele ya waandishi wa habari kuwa wamemsajili Niyonzima baada ya kumaliza mkataba na timu yake Yanga.

Mbali na nyota hao inasemekana pia mshambuliaji Nicholas Gyan raia wa Ghana ni miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kutambulishwa siku ya tamasha hilo huku chanzo chetu kikipasha kuwa atawasili usiku wa leo.

Kila mmoja aligoma kuzungumza na waandishi wa  habar ambao walikuwepo uwanjani hapo hadi saa 11 alfajiri wanafahamu kuwa viongozi wa Simba walijaribu kuzungumza na uongozi wa uwanja wa ndege ili Niyonzima na Okwi watokee kwenye mlango wa watu maalum (VIP) kwa lengo la kuwaficha ili wasimulikwe na kamera.

Mapema mchana wa jana Okwi aliweka picha kwenye mtandao wa Instagram inayomuonyesha akiwa na kipa Aishi Manula ndani ya ndege lakini ndege hiyo ilipotua Dar hakuonekana na hakuna mchezaji wala kiongozi aliyekuwa tayari kusema ‘alipopotelea’ nyota huyo kipenzi cha watoto wa Msimbazi.
     SOURCE:BOIPLUS

Post a Comment

 
Top