Dar es Salaam. Kaimu rais wa Simba, Salim Abdallah amewaomba wanachama wa Simba kupitisha mabadiliko ya uendashaji wa klabu yao.

Salim ameyasema hayo katika hotuba yake ikiwa ni muda mfupi kabla ya wanachama kupigia kura mabadiliko hayo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Wanachama zaidi ya 1,000 wamehudhuria mkutano huo ambapo Kaimu Rais wa Simba amesema endapo watapitisha mabadiliko hayo itatangazwa tenda.

SOURCE:MWANASPOTI

Post a Comment

 
Top