Ujio wa kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima ndani ya klabu ya Simba kunatazamiwa kuja kuleta changamoto kubwa kwa baadhi ya wachezaji ambao walikuwa na nafasi kubwa ya kucheza kwa msimu uliopita
Niyonzima ana uwezo wa kukupa vitu vitatu kwa wakati mmoja ndani ya kikosi, ni mzuri kwenye kutengeneza nafasi za kufunga, kuunganisha timu kuanzia eneo la ulinzi hadi la ushambuliaji pia kiungo huyo ana uwezo mkubwa wa kufunga magoli katika mazingira tofauti tofauti
Kwa sifa hizo ni dhahiri shairi kuna nyota wengi ndani ya wanaenda kuhathirika moja kwa moja kutoka na uwepo wa Haruna NiyonNiyonzimau Simba , FigFigisutzakuletea baadhi ya wachezaji ambao wataathirika kutokana na ujio wa NiyonzimNiyonzimaa SimSimbaSimbaNdemla
Nafasi yake itazidi kuwa ngumu maradufu kwa msimu ujao, kwani nafasi zote anazocheza Ndemla, Haruna Niyonzima uzimudu kwa ufanisi mkubwa, hivyo uwepo wa Mnyarwanda huyo ni kama kuja kumchimbia shimo Ndemla.
Jonas Mkude
Mkude anaweza kuaathirika endapo mwalimu Joseph Omog ataamua kutumia kiungo mkabaji mmoja na Niyonzima kutumika kama namba nane kwenye mifumo ya (4-4-2 au 4-1-4-1) , kuna nafasi kubwa mwalimu kuanza na James Kotei pamoja na Haruna.
Muzamiru Yasin
Mmoja wa wachezaji bora wa klabu ya Simba kwa msimu uliopita, Muzamiru anaitaji kufanya juhudi kubwa kwa msimu ujao ili kupata nafasi mbele ya Niyonzima, wana uwezo wa kucheza pamoja endapo Omog atawatumia wote ila mwalimu akiamua kumtumia mmoja wapo kuna nafasi kubwa ya Yasin kuanzia benchi.
Mo Ibrahim
Amekuwa akitumika kama kiungo wa pembeni upande wa kushoto karibu msimu mzima, bado siyo salama kwake maana Niyonzima pia amekuwa akitumika kushoto na kufanya vizuri sehemu ambayo hata kwenye klabu yake ya zamani ya Yanga alitumika sana.
Laudit Mavugo
Mrundi huyo naye ni mmoja wa wahanga wa ujio wa Haruna Niyonzima kwani mwalimu akihamua kutua mshambuliaji mmoja na Haruna kuchezeshwa nyuma ya mshambuliaji huyo, kuna uwezekano wa Omog kuwatumia Bocco na Haruna kwenye eneo la ushambuliaji, nafasi ya Mavugo ni Omog kuanza na washambuliaji wawili huku Mrwanda
Post a Comment